Huduma zote za Google, zinakufanyia kazi

Ingia katika Akaunti yako ya Google ili ufurahie zaidi huduma zote za Google unazotumia. Akaunti yako hukusaidia ufanye mambo mengi kwa kuweka mapendeleo kwenye hali ya utumiaji katika Google na kukupa uwezo wa kufikia taarifa zako muhimu kwa njia rahisi mahali popote.

Inakusaidia

Unapoingia katika akaunti, huduma zote za Google unazotumia hufanya kazi kwa pamoja ili kukusaidia kutekeleza majukumu ya kila siku kama vile kusawazisha akaunti yako ya Gmail na programu za Kalenda na Ramani ya Google ili kuhakikisha kila wakati unafuata ratiba vyema.

Zimebuniwa kwa ajili yako

Bila kuzingatia kifaa au huduma ya Google unayotumia, akaunti yako hukupa hali nzuri ya utumiaji ambayo unaweza kudhibiti na kuwekea mapendeleo wakati wowote.

Inakulinda

Akaunti yako ya Google inalindwa kwa vipengele bora vya usalama ambavyo husaidia kutambua na kuzuia hatari kiotomatiki kabla hazijakufikia.

Tayari kukusaidia

Tayari kukusaidia

Huduma za Google, kuanzia Chrome hadi YouTube, hufanya kazi vyema na hukusaidia kufanya mambo zaidi ukiwa umeingia katika akaunti. Akaunti yako hukupa uwezo wa kufikia vipengele vinavyoweza kukusaidia kama vile Kujaza kiotomatiki, mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo na zaidi — wakati wowote kwenye kifaa chochote.

Kwa ajili yako

Kwa ajili yako

Akaunti yako ya Google hufanya kila huduma unayotumia ikufae. Ingia tu katika akaunti yako ili ufikie vidhibiti vya kuweka mapendeleo na faragha kwenye kifaa chochote.

Kulinda taarifa zako kwa njia salama na ya faragha

Kulinda taarifa zako kwa njia salama na ya faragha

Hatua ya kulinda taarifa zote katika Akaunti yako ya Google ni muhimu zaidi. Kwa hivyo, tumeweka zana na ulinzi thabiti kama vile Ukaguzi wa Usalama na Kidhibiti cha Manenosiri cha Google katika kila akaunti.

Huduma zako za Google zinaanzia hapa